Friday, January 22, 2010
Tishio la Majembe Dawasco lakusanya bil. 8/- kwa wiki
SIKU sita baada ya kampuni ya Majembe Auction Mart kutangaza kuanza operesheni ya kukata maji na kukusanya madeni ya Mamlaka ya Maji Dar es Salaam (DAWASCO), baadhi ya wateja waliokuwa wakidaiwa wamelipa sh. bilioni nane na kupunguza deni la awali kutoka sh. bilioni 28 hadi sh. bilioni 20.
Alhamisi iliyopita, kampuni ya Majembe maarufu kama Vijana wa Kazi, walitangaza operesheni ambayo ingeanza jana Dar es Salaamu, na kabla ya kuanza kwake wadaiwa wengi sugu walimiminika Dawasco na kulipa zaidi ya Sh bilioni nane.
Katika siku ya kwanza ya operesheni hiyo itakayodumu kwa mwezi mmoja, nyumba sita zilikatiwa maji na Mkurugenzi Mtendaji wa Majembe, Bw. Sett Motto alisema kuwa walengwa ni wateja waliojiunganishia maji na wadaiwa sugu ambao watakatiwa maji.
"Kwa leo tunataka wananchi wajue kuwa zoezi lipo na ni endelevu, tumeanza kwa nyumba chache na leo tuapita nyumba kwa nyumba ili kubaini wanaotumia maji bila kulipa," alisema Bw.Motto
Bw. Motto alisema wananchi watakaowafichua waliojiunganishia maji watapewa zawadi ya sh. 5,000,000,ambapo kwa wadaiwa sugu watakaojitokeza kulipa bili zao watapunguziwa kiasi kidogo.
Aidha alisema kwamba lengo la kufanya hivyo ni kuipunguzia madeni DAWASCO kutokana na wengi kushindwa kulipa bili kwa wakati, hivyo kulifanya shirika hilo kuingia hasara kubwa.
Ofisa Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Mary Lyimo alisema kuwa wateja wengi wamekuwa na tabia ya kukaa kwa muda mrefu bila kulipa madeni na kusababisha kukosekana kwa matengenezo ya baadhi ya miundombinu nchini.
"Wateja 4,000 ni wadaiwa sugu, wengi wao wanadaiwa milioni 1 na kuendelea, hii inatupa sana tabu katika ufatiliaji lakini tunaamini majembe watatusaidia zaidi katika operesheni hii," alisema Bi. Lyimo
Baadhi ya wadaiwa sugu waliokatiwa maji jana ni pamoja na Bw. Makua Chombo mtaa wa Elikoma Kariakoo anayedaiwa sh 1,458,000, kampuni ya Fazal Communication (Sofia House) iliyopo Livingstone Kariakoo inayodaiwa sh. 2,445,964 na Bw. Juma Salim wa Mtaa wa Udoe Kariakoo anayedaiwa Sh. 1,016,800.
Friday, November 20, 2009
TRA Yapiga Kofuli Mitambo
MAMLAKA ya Mapato nchini(TRA) kupitia wakala wake wa ukusanyaji madeni sugu kampuni ya Majembe Auction Mart"Vijana wa Kazi"jana walipiga kufuli mali za kampuni ya kufua umeme ya Dowans kutokana na TRA kuidai kampuni hiyo Sh 9,120,611,746 ya kodi zake balimbali.
Akizungumza kupitia kituo cha televisheni cha taifa(TBC1) jana,Afisa Masoko wa Kampuni ya Majembe Action Mart,Dixion Kitime alisema hatua hiyo imechukuliwa kufuatia kampuni hiyo kushindwa kulipa kodi ya kiasi hicho cha fedh kwa muda mrefu.“Tumekamata mitambo ya Kampuni ya Dowans leo(jana)asubuhi na kuanzia sasa inashikiliwa na kampuni yatu kwa kushindwa kulipa deni lake la muda mrefu,”alisema Kitime.
Kitime alitaja baadhi ya mitambo iliyokamatwa kuwa ni makontena nane ya kuhifadhia mafuta pamoja na mitambo mingine.Alifafanua kuwa mitambo hiyo imekamatwa ili kuwalazimisha wamiliki wake kulipa gharama za Sh 9 bilioni wanazodaiwa na TRA na kusisitiza kuwa kama hawatafanya hivyo ndani ya siku 10 kuanzia leo mali hizo na mitambo itapigwa mnada hadharani. Habari imeandikwa na Geofrey Nyang'oro.
Sumatra Yaiteua Majembe Auction
Katika kuimarisha usimamizi wa utoaji huduma za usafiri na kuondoa kero kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam,Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Mjini(SUMATRA) imeteua Kampuni ya Majembe Auction Mart kuwa wakala wake wa kufuatilia utekelezaji wa masharti ya leseni ya usafirishaji abiria kwa mabasi yanayotoa huduma ya usafiri katika Mkoa wa Dar es Salaam(Daladala)na pia mabasi ya Mikoani yanayoanzia Kituo Kikuu cha Ubungo.
Kampuni ya Majembe Auction Mart ambayo imeteuliwa kufanya kazi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja itatekeleza majukumu waliyopewa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani.
Moja ya majukumu makubwa ya Kampuni hiyo itakuwa ni kusimamia na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa mabasi ya Daladala yanayotoa huduma katika Jiji la Dar es Salaam na viunga vyake ili kuhakikisha kuwa masharti ya leseni ya usafirishaji abiria yanafuatwa na watoa huduma ili hatimaye huduma ya usafiri katika Jiji iwe bora na yenye kukidhi mahitaji na matarajio ya wakazi wa Dar es Salaam.
Ili huduma ya usafiri katika Jiji iendelee kuwa bora zaidi,ni matarajio ya Mamlaka kuwa wamiliki,madereva pamoja na makondakta wa mabasi ya Daladala watatoa ushirikiano unaostahili kwa Majembe Auction Mart na Kikosi cha Usalama Barabarani wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.Aidha wadau na wananchi kwa ujumla wanaombwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa mamlaka zinazosimamia usafiri pamoja na Kampuni ya Majembe kwa lengo la kuimarisha usimamizi na kuboresha huduma hii muhimu kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.
Mamlaka ya SUMATRA itafuatilia na kusimamia kwa karibu sana utendaji wa wakala Majembe Auction Mart kwa mujibu wa Sheria na Taratibu ili kuondoa kero za usafiri kwa wakazi wa Dar es Salaam.Tuchukue fursa hii pia kuwakumbusha wananchi kupunguza purukushani kwa kupanga mstari wakati wa kupanda mabasi.
Wednesday, September 12, 2007
UFUNGUZI WA BLOG YETU
Tunatoa shukrani zetu kwa wateja wote waishio nje na ndani ya nchi yetu.Napenda kuwakaribisha wote duniani kwenye blog yetu. Kwa mahita yenu yote katika uuzaji na ununuzi wa vitu vipya na vya zamani , kama nyumba, magari, computer ,nk, wasiliana na .............VIJANA WA KAZI.. ....................SETH MOTTO ........ Mkurugenzi wa Majembe Auction Mart .
Subscribe to:
Posts (Atom)